Jumamosi, 19 Oktoba 2013

HABARI KATIKA PICHA: AIRPORT RANGERS FC 0-0 MUUNGANO FC. LIGI DARAJA LA TATU

Mchezo wa mpira wa miguu katika ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa  uliendelea kulindima katika viwanja mbali mbali hapa mkoani mbeya siku ya jana tarehe 18.10.2013 , timu ya airport rangers imejikuta ikilazimisha sale ya bila kufungana na timu ya Muungano f.c kutoka Tukuyu mbeya.

Mchezo huu ulijaa lawama nyingi kwa muamuzi wa mchezo kwani alionekana wazi hakua na vigezo vya kuchezesha mpira pale alipo onekana aki fanya maamuzi yasiyo ya kimchezo, mfano vijana wa Muungano kipindi cha pili walipiga shuti kali kuelekea goli la airport rangers mpira huo ukaelekea nje ya uwanja sentimita chache na mwamba wa juu lakini cha kushangaza muamuzi aka puliza kipyenga kwamba ni goli na wakati kulikua na nyavu golini na kama linge kua gori basi m,pira ungebaki ndani ya nyavu...

pili kupulza firimbi ya kutoa adhabu pale ambapo hakuna kosa lilio tendeka



vijana wa airport rangers wakiweka mwili safi dakika chache kabla mchezo kuanza katika uwanja wa magereza siku ya jana mnamo majira ya jioni
waamuzi wakitoa msisitizo juu ya nidham kwa manahodha wa  timu zote mbili dk chache kabla ya mchezo kuanza


kikosi cha timu ya Airport rangers kilicho lazimishwa sale ya kuto fungana na timu ya Muungano toka tukuyu hapa mkoani mbeya katika uwanja wa magereza , Kwa majina tukianza na walio simama kutoka kushoto ni Lukelo, kilongo, Aswile, Edward, Sabebe,Mwalugala na tukianza na walio weka mikono kwenye magoti kutoka kulia , Robert, Jimmy, Alex, Amri na Thomas

kikosi cha timu ya muungano kutoka busokelo tukuyu kilicho jawa na wachezaji walio kua sumu ya vijana wa airport kupata ushindi
waamuzi walio pewa dhamana na  M.R.E.F.A  kuchezesha mchezo wa ligi daraja la tatu baina ya Airport rangers fc na Muungano fc ktk uwanja wa magereza wakiongozwa na muamuzi wa kati MR. japhet
uongozi wa timu ya Air poart rangers fc ukitafakari mchezo ulio kua mbele yao dk chache kabla ya mchezo
wazee wanamichezo wakiongozwa na diwani wa kata ya iyela Charles Nkela (katikati ) walipo fika uwanjani kutizama namna vijana wao wa kata ya iyela wakicheza mpira ( sera mpira ni furaha na mpira ni ajira). mwisho wa mchezo wote vichwa chini kisa vijana hawakufanikiwa kuondoka na ushindi..... Air port rangers msiangushe wadauuuuuuuuu!!!!!!.

0 maoni:

Chapisha Maoni