Jumanne, 27 Agosti 2013

KIOO CHETU

Hakuna raha kama kua na kioo  sababu, kina raha yake maana hauwezi kutembea na uchafu ukijitizama  lazima ujisafishe ,,, hapa namuona kijana wetu ambae ni kijana wetu katika soka (Jimmy Shoji)  akiwania mpira na mchezaji maarufu sana tanzania ( Mrisho Ngasa)... hapa ilikua ni mechi kati ya jkt luvu na simba ambapo kaka huyu ambae wengi tumekua tukimfaham kwa jina la Gema aliongozana na wachezaji wenzake wa jkt ruvu stars kulazimisha suruhu ya 1-1 ,, ndugu zangu  kwangu hiki ni kiioo kwetu haswa Sie wapenda soka la maendeleo
Nafasi yake uwanjani
Bwana shoji anapendelea sana kucheza kama kiungo mkabaji ,namba sita (6)  namba hii kwake ni kama nyumbani maana hujisikia faraja na ni namba ambayo akicheza ni nafasi kubwa kwake kuonyesha mafanikio katika timu husika ..
Historia yake mpira
Bwana Shoji hakuanza mpira hewani na hii ni safari yake ya mpira kwa mda wa miaka kadhaa iliyo pita na timu alizopitia
1.      Alizaliwa mwaka           1993,
2.      Aliichezea                       airport junior
3.      Aliichezea                       Forest Youth Academy (foysa)
4.      Aliichezea                       Tanzania Prison ( II)
5.      Aliichezea                        AFC Arusha tokea  2008 hadi 2010
6.       Aliichezea                      JKT RUVU stars tokea 2011 hadi  may 2013
7.       Anachezea                  Tanzania prisons kwa msimu wa 2013-2014 akiwa kama mchezaji mpya  alie sajiliwa june 2013
mashindano aliyo wahishiriki
1.      Kombe la muungano akiwa na forest youth academy (foysa)
2.      Taifa cup akiwa na AFC arusha 
3.      Rolling stoney cup
4.      Ligi daraja la kwanza AFC arusha
5.       Ligi kuu vodacom (VPL) kwa misimu miwili akiwa  AFC arusha na baada ya hapo akahamia JKT  ruvu stars, na sasa akiichezea Tanzania Prison SC
mataji na medali alizo wahichukua
1.      mchezaji bora taifa cup , arusha na tanga
2.      rolling stone cup, medali moja akiwa na   foysa kama  mshindi wa tatu


0 maoni:

Chapisha Maoni