Mgawanyo wa sh Mil 102/-
|
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Ashanti United
iliyochezwa (Agosti 24 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
imeingiza sh. 102,856,000.
Watazamaji 17,744 walikata tiketi kushuhudia mecchi hiyo namba
moja ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa mabingwa watetezi Yanga
kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-1.
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000,
sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 24,400,102.45 wakati
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 15,689,898.31.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh.
12,406,831.75, tiketi sh. 4,453,890, gharama za mechi sh. 7,444,099.05, Kamati
ya Ligi sh. 7,444,099.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
3,722,049.53 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
2,894,927.41.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 maoni:
Chapisha Maoni