Jumapili, 8 Septemba 2013

MCHEZO WA KIRAFIKI KATI YA AIRPORT RANGERS FC VS MBASPO FC KUCHEZWA LEO TAREHE 08.09.2013


B
aada ya mchezo wa kirafiki kati ya mbeya city na airport rangers kusogezwa Mbele mpaka hapo tarehe  10.09.2013 kwa sababu zilizo nje ya uwezo wa waandaaji wa mchezo huo…

M
abingwa katika kombe la muungano  julai 2013 timu ya Mbaspo kutoka Mbeya leo jumapili panapo majira ya saa 10 kamili Katika uwanja wa Magereza wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Airport Rangers FC
H
ii ni moja ya mbinu za uongozi wa airport rangers kuinoa timu yao kwa kucheza na timu ambazo zinaushindani ili kuweza kupata picha timu hii ipo katika hali gani kabla ya mashindano yanayo tarajia kuanza hapo tarehe 4.10.2013
K
wani  baada ya kufanikiwa kushinda kwa mikwaju ya penati 5-4 dhidi ya wahasimu wao Mbeya City vijana wa Mbaspo katika mashindano hayo ya kombe la muungano walifanikiwa kunyakua kombe na pesa kiasi cha Tsh milioni 3
AIRPORT RANGERS FC USHINDI JADI YETU







Maoni 2 :

  1. Ngapi ngapi Mbaspo na Airport Rangers?

    JibuFuta
    Majibu
    1. hllowww,,, chriss,,mechi hii ya kirafiki iliishia kwa tim zote mbili kuchoshana nguvu pale ambapo mpaka refa wa mchezo anapuliza kipyenga hakuna tim ilofanikiwa kuliona rango la mwenziee,,, ingaw a mchezo ulikua wa kubamba ile mabaya

      Futa