USHINDI JADI YETU
|
Vijana wa Airport rangers wakiwa katika mazoezi ya viungo katika uwanja wa uhasibu mjini mbeya
ikiwa ni mfululizo wa mazoezi kama moja ya maandalizi ya ligi ya mkoa (mbeya) 2013.
ligi hiyo ikiwa inatarajiwa kuanza mapema mwezi wa kumi na kurindima katika
viwanja mbalimbali katika mkoa huu wa mbeya.
Vijana wanakila sababu za kuvuka kwenda katika ligi ngazi ya
taifa kwani timu imesheheni wachezaji wenye uwezo wa hali ya juu na nidham ya pekee
, kwani hufanya mazoezi kwa pamoja,vijana hawa wamekua wakionyesha mabadiliko
chanya kimpira kadiri siku zinavyo zidi kwenda Mbele, huwai kufika mzaoezini
mapema kama kocha wao awaelekezavyo nani vijana wenye usikivu wa namna yake
pale wanapo pewa maelekezo na waalim wao.
Mazoezi hufanyika kila siku kuanzia jumatatu mpaka jumamosi
katika uwanja wa uhasibu kuanzia saa 10 kamili mpaka saa12 kamili jioni, wape
support vijana hawa hata kwa kufika uwanjani kutizama kile wakifanyacho kama
wachezaji mda huo wa join katika siku za juma.
Bwana Yusuph Mlekwa na kijana Boaz Mwakibete ndio waalim wakuu waliopewa
dhamana ya kuifundisha timu hii kwa
kipindi hiki kigumu cha maandalizi mpaka hapo baadae.

0 maoni:
Chapisha Maoni