Nahodha wa timu (majeruhi) bwana Robert wakwanza kulia akiwa na mwalimu wa timu bwana Yusuph mlekwa (wapili toka kulia) bila kumsahau kocha msaidizi bwana Boaz (wa pili kushoto ) na team manager (wakwanza kushoto) wakiwa uwanjani (MAGEREZA) wakitizama mchezo wa kirafiki kati ya airport rangers fc vs Chuma chakavu fc ambapo timu ya Airport rangers imefanikiwa kuondoka na ushindi mwembamba wa bao moja kwa nunge
Hapa kazi tuuu mzee wa shughuli (sabebe) akiwa katika harakati za kuhakikisha timu yaondoka na ushindi baada ya kuchezea kichapo dhidi ya mbeya city
hiii sijui ndio man to man? lakini yote heri jamaa anakaba kwa kila mbinu
kibongo bongo haya ndio twakumbana nayo katika soka ,,,, vijana sita na wote wapo eneo moja la mpira.... hii hata Maksimo hajawahi fundisha... sio mbaya mala moja moja sio mbaya
mathew usikabie macho baba utauza timu ... sio mbaya fair play kaka nimeona leo ingawa pole kwa mchezo mbaya walokuchezea
Half time: vijana wakitumia murua dakika kumi na tano kabla refarii haja puliza kipyenga cha ngwe ya pili wakijaribu kurekebishana kwa makosa yaliyo weza jitokeza katika kipindi cha kwanza kwani ngoma ilikua bila bila.
Vijana wakichukua maelekezo kutoka kwa mwalimu (yusuph Mlekwa) baada ya kipindi cha kwanza kumalizika kwa matokeo ya bila kufungana ''Mpendane, mtumane , na muheshimiane uwanjani" yakiwa ni maneno toka kwa mwalimu kuwafanya vijana wawe na moyo wa kujituma na moyo wa ushindi wawapo uwanjani
bwana Amir (striker) alie ingia kipindi cha pili kuongeza kasi ya mchezo ilio zaaa matunda ya bao moja lilo fungwa na mchezaji nambali tisa (Yonah) akitokea nje ya uwanja .
hapa kazi tuu
AIRPORT RANGERS FC : USHINDI JADI YETU DAIMA

0 maoni:
Chapisha Maoni